Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) zatiliana saini mkopo wa Bilioni 361.71.

Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) zimetiliana saini mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 130, sawa na shilingi bilioni 361.71 kwa ajili ya kujenga mitambo ya kuzalisha umeme wa jua Megawatt 150 Wilaya ya Kishapu,Shinyanga. Mradi huu ni wa mwaka mmoja  ambao unatarajiwa kuanza mwezi machi 2022 na